Gundi (mnyama)
Gundi | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Gundi
| ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
|
Gundi (kutoka Kiingereza: gundi) au panya-kichanuo (kutoka Kiingereza: comb rat) ni wagugunaji wadogo wa familia Ctenodactylidae wanaotokea kaskazini kwa Afrika. Huishi katika majangwa yenye miwamba. Mwili wao ni mnono wenye urefu wa sm 17-18 na unafunikwa kwa manyoya laini. Wana miguu mifupi, macho makubwa na mkia mfupi. Miguu yote ina vidole vinne tu na vile vya kati vya miguu ya nyuma vina nywele ngumu zinazofananana na kichanuo (sababu ya jina la panya-kichanuo). Hula kila aina ya mmea ipatikanayo, lakini, kama wanyama wengi wa jangwa, hawakunywi na hupata maji yote wanayoyahitaji kutoka chakula chao[1]. Jike huzaa watoto wawili kila mara baada muda wa mimba wa mieze miwili. Kwa sababu ya uhitaji wa kuhifadhi maji jike hutoa maziwa machache tu na watoto hulikizwa kabisa baada ya wiki nne.
Gundi huishi katika makoloni ya wanyama hadi mia moja au zaidi, lakini idadi ni ndogo katika maeneo ambapo chakula ni adimu. Hawatengenezi matundu ya aushi lakini hujisitiri katika mianya ya miamba usiku au mchana wakati wa joto kubwa. Wanyama hawa hufanya sauti sana na wana namba ya sauti za alamu na mawasiliano ambazo zinawasaidia kwa kugundisha makundi yao.
Spishi
- Ctenodactylus gundi, Gundi Kaskazi (Common au North African Gundi)
- Ctenodactylus vali, Gundi wa Val (Val's au Desert Gundi)
- Felovia vae, Gundi wa Felou (Felou Gundi)
- Massoutiera mzabi, Gundi wa Mzab (Mzab Gundi)
- Pectinator spekei, Gundi wa Speke (Speke's Gundi au Pectinator)
Marejeo
- ↑ Macdonald (Ed), Professor David W. (2006). The Encyclopedia of Mammals. Oxford University Press. ISBN 0-19-920608-2.
{{cite book}}
: Cite has empty unknown parameter:|coauthors=
(help)