Mkuyu
Mkuyu (Ficus spp.) | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mkuyu mwangajo (Ficus sur)
| ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Kadiri ya spishi 800 |
Mikuyu ni miti ya jenasi Ficus. Kwa kawaida hiyo ni miti mikubwa. Maua, na hivyo matunda pia, huota kutoka shina na matawi makubwa. Matunda huitwa makuyu.
Kuna kadiri ya spishi 800 za mikuyu. Mkuyu unaopandwa na ambao matunda yake huliwa sana, una jina lake: mtini, na matunda yake matini.
Makuyu si matunda halisi. Tabaka la nje ni sehemu ya tawi iliyojifunga katika tufe na huitwa sikonio (syconium). Mkabala na kikonyo kuna tundu dogo liitwalo ostioli. Maua yamo upande wa ndani wa ukuta wa sikonio. Uchavushaji wa maua hufanyika na nyigu wadogo sana (nyigu-makuyu). Jike la nyigu, ambao ametoka kwenye sikonio nyingine na amepambwa na chavua, aingia kupitia tundu dogo kwa nguvu akipoteza mabawa yake. Halafu ataga mayai katika ovari za maua na sawia achavusha stigma. Baada ya kutoka kwenye mayai lava wala tishu za maua. Madume wakiwa wamekuwa wapevu hawana mabawa na wapanda majike tu. Halafu watoboa tundu katika sikonio ili kuacha majike watoke na baadaye madume wafa. Kila spishi ya mkuyu ana spishi yake (au zake) ya (za) nyigu maalum.
Katika Biblia
Nabii Amosi alikuwa analima mikuyu (Am 7:12-15), lakini mti huo umepata umaarufu kutokana na Zakayo kupanda juu yake ili kumuona Yesu akipita mjini Yeriko (Lk 19:1-10).
Spishi zilizochaguliwa
- Ficus benghalensis, Mkuyu Baniani (Banyan)
- Ficus benjamina, Mkuyu Mwinamo (Weeping fig)
- Ficus bussei, Mkuyu Mtamba (Zambezi fig)
- Ficus carica, Mtini (Common fig)
- Ficus elastica, Mkuyu Mpira (Rubber fig)
- Ficus exasperata, Mkuyu Msasa (Forest sandpaper fig)
- Ficus lingua, Mkuyu Mkechere (Boxwood fig)
- Ficus natalensis, Mkuyu Mlandege au Arabi (Barkcloth fig)
- Ficus sur, Mkuyu Mwangajo (Cape fig)
- Ficus sycomorus, Mkuyu Chivuzi (Sycomore fig)
- Ficus tremula, Mkuyu Mvumo (Quiver-leaf fig)
Picha
-
Mwangajo: majani
-
Mwangajo: makuyu mtini
-
Mwangajo: kuyu lililopasuka
-
Nyigu-makuyu juu ya kuyu la mwangajo