Nenda kwa yaliyomo

Solomon kaDinuzulu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
The printable version is no longer supported and may have rendering errors. Please update your browser bookmarks and please use the default browser print function instead.

Solomon kaDinuzulu (18911933) alikuwa mfalme wa taifa la Wazulu kuanzia mwaka 1913 hadi kifo chake kilipowadia mnamo tarehe 4 Machi ya mwaka wa 1933 mjini Kambi. Solomo alizaliwa katika kisiwa cha St. Helena wakati huo baba yake alikuwa hapo kiuhamishoni.

Kuunganika kwake na ANC akawa ndio mwanzilishi halisi wa chama cha Inkatha (au Inkatha kaZulu kama ilivyokuwa inajulikana) mnamo mwaka wa 1920. Chama kilianzishwa kuwa kama kinapinga sera zilizopo dhidi ya waziri mkuu wa wakati huo, bwana Jan Smuts, na sera zake za kutaka kutoa msaada katika taifa lao mnamo mwaka 1920.

Moja kati ya dada wa Solomoni alikuwa binti wa mfalme aliyekuwa anafahamika kwa jina la Constance Magogo, ambaye alikuja kuwa maarufu sana kwa kuimba nyimbo za asili ya Kizulu, vile vile kuwa mama wa mwanaharakati na kiongozi wa chama cha Kizulu (Inkatha Freedom Party-IFP) bwana Mangosuthu Buthelezi.

Solomoni alifuatiwa na mtoto wake wa kiume aitwaye Cyprian Bhekuzulu kaSolomon.