Nenda kwa yaliyomo

Norwei

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Norway)
Kongeriket Norge
Kongeriket Noreg

Ufalme wa Unowe
Bendera ya Unowe Nembo ya Unowe
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: Alt for Norge ("Yote kwa Unowe" ni wito wa kifalme)
Kiapo kufuatana na katiba ya 1814 : "Enige og tro til Dovre faller" ("Pamoja na waaminifu hadi milima ya Dovre inaporomoka")
Wimbo wa taifa: Ja, vi elsker dette landet

Wimbo wa kifalme: Kongesangen
Lokeshen ya Unowe
Mji mkuu Oslo
59°56′ N 10°41′ E
Mji mkubwa nchini Oslo
Lugha rasmi Kinowe1
(Bokmål na Nynorsk)
Serikali Ufalme wa kikatiba
Harald V
Jonas Gahr Støre
Katiba
Uhuru
Ilitangazwa
Ilitambuliwa

Kutoka maungano na Uswidi
7 Juni 1905
26 Oktoba 1905
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
385,207 km² (ya 673)
{{{percent_water}}}
Idadi ya watu
 - 2024 kadirio
 - 2013 sensa
 - Msongamano wa watu
 
5,550,203[1] (ya 116)
5,136,700
14.4/km² (ya 213)
Fedha Krone ya Unowe (NOK)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
CET (UTC+1)
CEST (UTC+2)
Intaneti TLD .no2
Kodi ya simu +47

-

1Lugha rasmi ya Kinowe inapatikana kwa namna mbili: bokmål zaidi kama lugha ya kimaandishi na Nynorsk zaidi kama lugha ya majadiliano ingawa inaandikwa pia. Lugha ya Kisami ni lugha rasmi katika miji 6 na Kifini katika mji mmoja.


Unowe (auː Norwe, Norwei; kwa Kinorwei Norge/Noreg; jina rasmi ni Ufalme wa Unoweː Kongeriket Norge kwa Bokmål na Kongeriket Noreg kwa Nynorsk) ni nchi ya Skandinavia katika Ulaya ya Kaskazini.

Imepakana hasa na Uswidi, ila katika ncha ya kaskazini na Ufini na Urusi pia.

Ina pwani ndefu kwenye Bahari ya Kaskazini na ya Atlantiki.

Visiwa vya Svalbard na Jan Mayen katika bahari ya Aktiki ni maeneo ya Norwei.

Pia visiwa visivyokaliwa na watu vya Bouvet katika Atlantiki ya kusini na Peter I katika Pasifiki ya kusini viko chini ya Unowe.

Nchi inadai pia sehemu ya Queen Maud Land katika bara la Antaktika penye kituo cha kisayansi cha Troll.

Mkuu wake kwa sasa ni Mfalme Harald V.

Bunge huitwa Stortinget na wanachama wake huchaguliwa na wananchi kila baada ya miaka minne.

Sikukuu ya taifa ni tarehe 17 Mei, ambapo husherekewa katiba ya Unowe ya mwaka wa 1814.

Mji mkuu ni Oslo, wenye wakazi wanaozidi 530,000. Miji mingine mikubwa ni pamoja na Bergen wenye wakazi 230,000 na Trondheim wenye wakazi 150,000; yote miwili imewahi kuwa miji mikuu ya Unowe katika miaka ya mwanzoni.[2]

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Nchi ilikaliwa na watu wawindaji-wakusanyaji tangu mwaka 10000 KK hivi.

Katika miaka 3000 - 2500 KK waliingia wakulima wa Kizungu.

Katika karne ya 8 hadi karne ya 10 Norwei ilipeleka mabaharia wake Waviking hadi mbali sana.

Kwa muda mrefu Norwei ilibaki katika muungano na Udani na Uswidi.

Ufalme umekuwa huru tangu mwaka wa 1905.

Unowe ilikuwa nchi maskini ya wakulima na wavuvi, lakini tangu kupatikana kwa mafuta ya petroli baharini imekuwa kati ya nchi tajiri kabisa duniani.

Takriban watu milioni 5.5 wanaishi nchini Unowe. Wengi wao (81.5%) ni Wanorwei asili, jamii ya Wajerumani. Asilimia 18.5 ni wahamiaji au watoto wa wahamiaji wawili (hasa Wapolandi, Walithuania, Wasomali, Wapakistani na Waswidi). Wengi wao sasa wana uraia wa Norwei.

Dini ya kwanza ni Ukristo (74.9%), hasa madhehebu ya Kilutheri (68%), halafu Wakatoliki (3.1%, hasa wenye asili ya Polandi). Hata hivyo wananchi wengi hawajali sana; wanaoshiriki ibada kila wiki ni 2% tu.

Katika dini nyingine, unaongoza Uislamu (3.1%) ulioletwa na wahamiaji kutoka nchi mbalimbali walioongezeka sana kuanzia miaka ya mwisho ya karne ya 20. 21.2% hawana dini yoyote.

  1. "Population, 2024-01-01" (kwa Kiingereza). Statistics Norway. 2024-02-21. Iliwekwa mnamo 2024-02-25.
  2. "Trondheim - the official website". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-06-08. Iliwekwa mnamo 2009-09-04.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Norwei kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.