Tamthilia Ya Kifo Kisimani

Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 14
 
 TAMTHILIA YA KIFO KISIMANI UTANGULIZI
Tamthilia ya Kifo Kisimani imeandikwa na kithaka wa Mberia. Toleo la kwanza la kitabu hiki ililikuwa mwaka wa 2001 na kina chapa nyingi hadi kufikia mwaka wa 2009.kimechapishwa na Marimba Publications Ltd.
 Anwani
 Anwani huwa ni jina la kitabu.Mwandishi amefaulu kutumia anwani’Kifo Kisimani’.  Anwani hii inaashiria kifo cha Mwelusi pale kisimani alipouliwa na Gege. Pia anwani hii inaashiria kifo cha Wanabutangi baada ya kukosa maji pale kisimani.Hii ni baada ya kanuni mpya za utekaji maji kutolewa amabazo ziliwanyima haki za kuteka maji. Maji ni uhai hivyo kupewa siku tatu za kuteka maji ni kunyimwa uhai yaani kifo.
Jalada
Jalada ni karatasi ngumu inayofunika kitabu ambapo jina la kitabu huandikwa.Katika tamthilia hii kuna picha ya mtu aliye na huzuni.Mtu huyu ni kama ako katika shimo. Hii inaashiria shimo la mateso ambalo Wanabutangi wametiwa na utawala mbaya wa Bokono na vibaraka wake. Kuna picha inayoashiria machea.Hii inaonyesha matumaini kwa Wanabutangi baada ya Mwelusi na wenzake kuanza harakati za mabadiliko.Rangi inayotumika kwa picha ni ya udongo, kuashiria rotuba ya Butangi.
DHAMIRA YA MWANDISHI
Kiini cha jambo au habari iliyoandikwa na mwandishi.Katika Kifo Kisimani Kithaka wa Mberia ananuia kuamsha au kumchangamsha msomaji kuhusu utawala mbaya na jinsi  ya kuleta mabadiliko na kuuondoa . Mwandishi anatetea haki za walionyanyaswa.Hivyo lengo kuu la mwandishi ni kuzindua  watu.
PLOTI
Huwa ni mtiririko wa matukio katika kitabu.Tamthilia hii ina onyesho kumi.Muhtasari  wa onyesho hizi ni kama ifuatavyo.
Onyesho la kwanza
 
 Mchezo unaanza asubuhi ambapo viti vimepangwa tayari kwa mkutano wa Bokono.Mwelusi ambaye ni kijan anaingia uwanjani.Mawazo yake yanadhihirika kupitia kwa sauti tunayosikia .Yanamkejeli Bokono kwa ubinafsi wake na kuwanyanyasa  wanabutangi. Kaloo anaingia uwanjani kwa kutayarisha ,anamwona Mwelusi na anadhani ni mmoja  wa waliohudhuria lakini Mwelusi anamwambia alikuwa anapita tu ni mawazo  yaliyomshika mguu.Kaloo anafurahi kwa kuwa Mwelusi anawaza juu ya Butangi si kama  vijana wengine wanavyo waza kuhusu anasa. Mwelusi anakubaliana naye na kuongeza kuwa ni wakati wa vita. Kaloo hakubaliani naye na anamuomba amfafanulie matamshi  yake. Mwelusi anamwambia kuwa atamueleza siku nyingine kwa kuwa hahudhurii mkutano na anaondoka. Mwelusi Batu anaingia kuukagua uwanja, anafurahishwa na viti.Anapoelezwa kuwa Mbutwe seremala aliyeunda viti anadai kulipwa Batu anasema aje amwone na amdai malipo ya mbuzi wawili.  Wanawake ndio watakaocheza katika mkutanowa Bokono Mtemi wa Butangi.Batu anasema kuwa mtemi akifurahi,wanawake watafurahi.Azena anaingia uwanjani ili kumsaidia kaloo kwa matayarisho. Batu anaapoondoka Atega anaingia akifuatwa na Mwelusi. Wanashukiwa kuwa wapenzi kwa kuwa kila mara wanaonekana pamoja.Naye kama Mwelusi, anawafahamisha hatohudhuria mkutano.Batu anaingia tena uwanjani na kuamrisha watu waitwe.Gege anaingia uwanjani huku akiwa anapuliza ala ya muziki. Batu anamwambia ni muziki wa kuvutia, yeye anasema kuwa anausifia uongozi wa busara wa Butangi. Kaloo anamhakikishai kuwa yeye na jamaa zake ni wazalendo kamili na hawatasita kuhudhuria mkutano. Batu anawasaidia kujitayarisha jinsi watamsifia Bokono;Bokono Bokono milele!! Baada ya muda kidogo wanagundua kuwa watu hawaji kwa mkutano.Kaloo anaenda Mingamiwili na kurudi lakini hakuwapata watu huko pia. Bokono anapofika anapata hakuna watu kwa uwanja anakasirika sana. Vibaraka wake  wanamuahidi kuwa kuna tatizo lakini watalinyoosha. Zigu anasema kuwa watu  wamechochewa na Mwelusi.Hata hivyo Batu anasema kuwa watamkomesha anayewachochea watu.Baada ya mabo kutulia wote wanaanza kumsifia Bokono ;Utaongoza Butangi kwa miaka mia moja.
Onyesho la pili
5
 
 Matukio ni katika makazi ya Mtemi Bokono amabayo ni sehemu ya majengo ya Utawala  wa Butangi.Bokono amesimama huku akiangalia vitu vilivyo ukutani na mara kwa mara anaguza hiki na kile.mkewe Nyalwe amekaa kitini raha mustarehe, akjipepea.punde Mgezi anakuja hadi alipo Nyalwe na kumuambia kuwa chakula kiko tayari.  Wanapokaa kula Bokono hali chakula ana wasiwasi sana. Nyalwe anapomuuliza ni kwa nini hali anamjibu kwa kejeli na kumuuliza juu ya vyeo vyake;mke, mwndani na msiri  wake. Nyalwe anamueleza Bokono kuhusu ndoto yake .Bokono anakubali kuwa ana hofu ya kunyang’anywa utawala.Nyalwe anamuomba abadilishe mienendo yake na anamuonya dhidi ya vibaraka wake wanoandanganya kuwa anapendwa na Wanabutangi. Bokono anapiga nduru kuwa amamwona nyoka ,anasema ameumwa na bafe lakini  wanagundua kuwa hamna nyoka mle ndani ni hofu tu ya Bokono. Nyalwe anampa Bokono habari kuhusu kijiji cha Mama Agoro ambao wangependa kuwagawia huzuni.Hii ni baada ya uwanja wao wa watoto kuchezea umepewa Askari mkuu.Mama Agoro aliahidi kuridi tena na tena kutetea haki yao.
Onyesho la tatu
Onyeshao hili ni katika gereza. Gereza ni chumba chenye kidirisha kimoja, kuta na sakafu chafu. Tunaonyeshwa mateso na dhuluma kwa Mwelusi kutoka kwa Mweke na Talui.  Wanaanza kwa kumita mtukufu mtemi anaponyamaza wanazidi kunchapa na kumsukuma hapa na pale. Mwelusi analalamika kuwa taya zake zinawaka moto kwani waliodai wamekuja kuzungumza naye wanafanya hivyo kwa mateke na makofi.  Wanamhoji Mwelusi na kumuuliza kama yeye ni mwelisi wa Biuki na kama anatoka kijiji cha Bunyanya na ukoo wa langile.Anapojibu wanamsifu kuwa yeye ni muungwana na ni kiongozi mzuri sana wa Butangi.  Wanamuuliza kama yeye ndiye kiongozi wa kundi la kabakaba.Wanazidi kumchapa ili aliri kuwa anahusika na shughuli za ukombozi lakini Mwelusi anakataa wanazidi kumachapa. Batu anaingia na kuwakataza kumchapa, anaomba nafasi azungumze na Mwelusi.
5
 
 Kwa upole anamshawishi Mwelusi akiri kuwa kiongozi wa wanamapinduzi na aombe msama kwa Mtemi Bokono. Mwelusi anapolia juu ya maumivu Batu anamwambia kuwa atapewa dawa nzuri akitoka gerezani baada ya kuomba msamaha.Batu anamuacha mwelusi peke yake kwani anadai kuwa akili ya binadamu hufanya kazi vizuri akiwa peke yake. Anaporudi na kupata  welusi hajafanya uamuzi .  Antaka akiri kwamba anatumiwa na majirani ili kuchafua Butangi. Anapotataa Btu anamwambia kuwa amepotoshwa . Batu anatoa ishara kwa Askari na kuondoka.
Sura ya nne
Onyesho hili linatokea mbele ya gereza.Andua amemletea ndugu yake chakula.Askari  wanamkataza kumuona na Askari 111 anajaribu kumdhurumu.Askari wanapanga kula chakula cha mfungwa lakini askari 1 anawakataza na kuwaomba wampe mfunwa chakula chake.anawaambia wenzake kuwa ni walafi.wanazungumza kuhusu utawala wa mtemi Bokono kama utafikia kilele au la.  Askari 11 anaeleza jinsi walijaribu kumgeuza mhutumiwa Fulani aache kuwa jiwe awe  binadamu.Walimng’oa kucha za mkono na za miguu, walimgeuza kuwa popo na  baadaye walifika katikati ya miguu yake na kupiga kambi hapo.badaye walimuua na kumzika msituni.
Onyesho la tano.
Onyesho hili ni nyumbani kwa Tanyauani.Tanya ameketi akidondoa nafaka katika uteo.Kwenye sehemu nyingine ya ua Gege amekaakaribu na uzio akiukaguakagua.punde anauachilia na kuanza kujishughulisha na utengenezaji wa ala ya muziki. Mamake anamuuliza kwa nini hajaenda kumtizama nduguye, Mwelusi kule gerezani.Gege anwambia mamayake asimzomee.Anaendelea kutengeneza ala na kusema kuwa wasichana watamtambua . Katika kumbukumbu zake Mwelusi anarejea na kumuuliza hali ya uwnaja wa ngoma.  Wazungumza kuhusu hali ya wanabutangi.Gege anamshuritisha nduguye kwa kujali  jamii kila mara na kusahau maisha yake mwenyewe. Mwelusi anamuomba aieonee huruma Butangi na awe mzalendao.  Andua anarejea nyumbani kutoka kisimani.Anajeraha upande mmoja wa uso  wake.Anamueleza mam yake kuwa hakupigana mbali amechapwa na Askari.  Azena anawatemebelea na kumtuliza Tanay juu ya mwanawe.Anamuomba asife moyo na azidi kumpelekea chakula.
5
5
5
5
5
5
5
5
5
5
5

Reward Your Curiosity

Everything you want to read.
Anytime. Anywhere. Any device.
No Commitment. Cancel anytime.
576648e32a3d8b82ca71961b7a986505