Ulimwengu Quotes

Quotes tagged as "ulimwengu" Showing 1-25 of 25
Enock Maregesi
“Hasira ni Shetani. Hekima ni Mungu. Kila kitu kimo ndani yetu. Hasira imo ndani yetu. Hekima imo ndani yetu. Atomu ni matofali ya ujenzi wa kila kitu ulimwenguni likiwemo jua na miili ya wanadamu. Ndani ya atomu kuna nguvu ya chanya na kuna nguvu ya hasi. Kama miili yetu imetengenezwa na atomu na katika kila atomu kuna nguvu ya chanya na kuna nguvu ya hasi, hivyo basi, tuna uwezo mkubwa wa kufanya mambo mazuri na tuna uwezo mkubwa wa kufanya mambo mabaya. Mtu akikutukana mwambie asante. Akikupiga mwambie asante. Akiendelea kukupiga, pigana. Geuza hasira yako kuwa hekima kwa faida yako na kwa faida ya wengine.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Potassium Cyanide si hatari inapokuwa nje. Ni hatari inapojichanganya na asidi za tumboni ambapo hubadilika na kuwa gesi ya 'hydrogen cyanide'. Gesi ya 'hydrogen cyanide' ni miongoni mwa sumu hatari zaidi ulimwenguni. Mtu akimeza kidonge cha 'cyanide' atapata madhara makubwa. Kichwa chake kitamuuma hapohapo na atachanganyikiwa akili. Ngozi yake itakuwa nyekundu, kwa sababu damu yake itakuwa nyekundu zaidi – kutokana na kuzidi kwa oksijeni katika damu. Mwili hautakuwa na uwezo tena wa kuchukua oksijeni kutoka katika damu ili uitumie, kwa hiyo damu itazidi kuwa na oksijeni zaidi. Atapumua kwa shida. Mapafu yake yatafanya kazi vizuri lakini mwili wake hautakuwa na uwezo wa kutumia oksijeni yoyote – hivyo atadhani ana matatizo katika mfumo wake wa kupumua. Atazimia. Yaani, oksijeni haitafika kwenye ubongo. Atapata kifafa na atatapika nyongo. Ubongo wake utashindwa kufanya kazi na atakuwa mahututi ndani ya sekunde kumi! Baada ya hapo moyo wake utasimama kufanya kazi, na atafariki dunia.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Tunazaliwa na kufa. Lakini hatujui tunakotoka. Wala hatujui tunakokwenda. Huenda tunatoka na kwenda katika dunia nyingine, ya ulimwengu mwingine, hivyo kutufanya wageni wa dunia yetu wenyewe. Acha dunia katika hali nzuri kuliko ulivyoikuta.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kiongozi wa kanda ya Afrika ya Kusini ya Tume ya Dunia Kamishna Profesa Justin Mafuru, alijitolea maisha yake kufanya vitu viwili vya msingi kwa ajili ya dunia: Kukomesha madawa haramu ya kulevya nchini Tanzania na duniani kwa jumla, kupitia Tume ya Dunia, na kutafuta kupitia maabara za CERN ('Conseil Européen pour la Recherche Nucléaire') chembe ndogo ya 'higgs' ('Higgs Boson') inayosemekana kuhusika na uzito ('mass') wa chembe ndogo kumi na sita za atomu kasoro chembe ya mwanga; iliyopotea mara tu baada ya mlipuko wa ulimwengu wa 'Big Bang', miaka bilioni kumi na tatu nukta saba iliyopita kwa faida ya uanadamu.”
Enock Maregesi, Kolonia Santita

Enock Maregesi
“Ndani ya sekunde moja baada ya ulimwengu wetu kuumbwa, miaka bilioni kumi na tatu nukta saba tano iliyopita, chembe zote ndogo zinazopatikana ndani ya atomu zilitengenezwa. Zote hizo zimeshapatikana isipokuwa 'Higgs Boson', na 'Higgs Boson' ndiyo ya muhimu kuliko zote.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Maisha ni kani au 'force' ya kipekee zaidi katika ulimwengu unaofahamika; achilia mbali changamani ('complexity') na kutapakaa ('diversity') zaidi kuliko kani zote! Ni tukio la ajabu kuliko matukio yote yaliyowahi kutokea.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kabbalah' ni sayansi ya Mti wa Uzima wa Milele wa Bustani ya Edeni au 'The Tree of Life of the Garden of Eden' katika mbingu ya nne, ambayo ni ramani ya ulimwengu na roho ya mwanadamu; au Sayansi ya Mungu, uchawi wa kujua 99% ya siri ya uumbaji wa Mungu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Wachawi wanamwabudu Shetani. Lakini Shetani wanayemwabudu si Shetani Ibilisi aliyeumbwa na Mwenyezi Mungu kuja kuudanganya ulimwengu wote. Ni Shetani roho ya mabadiliko, mabadiliko ya kweli, ya ufahamu kamilia ulimwengu huu ambamo sisi sote tunaishi. Wachawi, kwa maneno mengine, wanaabudu miungu – kama vile Inanna wa Mesopotamia, Isis wa Misri, Asherah wa Kaanani au Belus wa Assyria ambaye ndiye mungu wa kwanza kuabuadiwa kama sanamu duniani – iliyotwaliwa na Shetani tangu misingi ya ulimwengu huu kusimikwa. Dhambi aliyotenda Shetani mbinguni ni ndogo kuliko dhambi wanazotenda wachawi duniani, ijapokuwa dhambi aliyotenda Shetani haitaweza kusamehewa na ndiyo maana Shetani hataweza kuwasamehe wanadamu. Ni jukumu letu kuwaita wachawi wote kutoka Babeli na kuwaleta katika ukweli kama kweli wanayemwabudu ni Shetani Ibilisi, Shetani Beelzebub, Shetani Asmodeus, Shetani Leviathan, Shetani Mammon, Shetani Amon au Shetani Belphegor ambao ni mabingwa wa kiburi, uroho, zinaa, wivu, fedha, hasira na uvivu duniani. Wachawi hawajui, na usipojua waweza kufa bila kujua.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Sayari yetu hujulikana kama Dunia na jua letu hujulikana kama Sol. Dunia imo ndani ya mfumo wa jua wa Sol. Mfumo wa jua wa Sol umo ndani ya mfumo wa jua wa Sol Sector au Solar Interstellar Neighborhood, kwenye wenzo wa Orion wa falaki ya Njiamaziwa, wenye mifumo ya jua zaidi ya 40 ikiwemo Alpha Centauri, Nemesis, Procyon na Sirius. Solar Interstellar Neighborhood imo ndani ya falaki ya Njiamaziwa yenye nyenzo nne zinazozunguka kwa pamoja na falaki nzima. Falaki ya Njiamaziwa imo ndani ya kishada (‘cluster’) chenye zaidi ya falaki 55 ikiwemo Andromeda, Leo A, M32 na Triangulum, kinachojulikanacho kama ‘the Local Galactic Group’. ‘The Local Galactic Group’ imo ndani ya mfumo wa kishada kikubwa zaidi kiitwacho Virgo Supercluster, chenye makundi zaidi ya 100 ya falaki. Virgo Supercluster imo ndani ya mfumo mwingine mkubwa zaidi wa vishada uitwao Laniakea (Local Supercluster) wenye vishada zaidi ya 500 vya falaki. Hapo ndipo mwisho wa ulimwengu wetu unaoweza kuonwa na wanasayansi wetu. Kutoka duniani mpaka Laniakea ni umbali wa kilometa bilioni trilioni 250, miaka bilioni 13.8 iliyopita.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Dunia – Mfumo wa Jua wa Sol – Solar Interstellar Neighborhood – Njiamaziwa – Local Galactic Group – Virgo Supecluster – Local Supercluster – Ulimwengu unaoonekana – Ulimwengu. Huu ndiyo ukoo wa dunia yetu. Chochote alichokifanya Yoshua kilitokea katika ukoo huu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Lakini kuna ndoto takatifu na kuna ndoto za kishetani. Ndoto takatifu hutokea wakati akili imetulia baada ya mwili wote kupumzika, kama ambavyo usiku unavyokuwa kimya na kila kitu kimetulia, karibu na saa za alfajiri, ambapo mfumo wa usagaji chakula unakuwa umemaliza kazi yake. Kipindi hicho malaika wa Mungu hutufunulia siri kuhusu ulimwengu huu, ili kwamba tutakapoamka asubuhi tuwe na baadhi ya maarifa yaliyojificha ndani ya maandiko ya vitabu vitakatifu; kwa sababu malaika wa Mungu ndiye anayetawala ufahamu wetu, kama ambavyo Mungu anavyotawala hiari yetu, na kama ambavyo nyota zinavyotawala miili yetu. Lakini kwa wale waliokomaa kiimani malaika mwema anaweza kuwafunulia siri wakati wowote, haijalishi wamelala au wameamka. Kwa ajili ya ujanja wa Shetani ndiyo maana Mungu hutufunulia siri zake, ili tujihadhari naye.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mfundishe mtoto wako maadili mema kwa miaka kumi na tatu, katika umri wa miaka kumi na tatu fikra za mtoto huanza kuwa na maono na utambuzi wa vitu mbalimbali na watoto katika umri huo wanao uwezo wa kuchambua dhana kadha wa kadha za kinadharia na hali kadhalika wanao uwezo wa kuchambua nadharia tata zisizokuwa na hakika na hata zile zenye hakika zisizokuwa tata, kabla hujamkabidhi kwa dunia. Ukimkabidhi mtoto wako kwa dunia kabla ya umri wa miaka kumi na tatu, kama vile kumpeleka katika shule ya bweni au kumpeleka akalelewe na watu wengine ambao si wazazi wake, yale ambayo hukumfundisha atafundishwa na ulimwengu. Mpeleke mtoto wako katika shule ya bweni au kuishi na watu wengine akiwa amefundishwa maadili mema. Kinyume cha hapo atafundishwa na shule au watu wengine kwa kudharauliwa, kuchukiwa na kuadabishwa.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kuna mambo yanatokea hapa ulimwenguni ambayo yanafanya nikiri uwepo wa Mungu kwa asilimia kubwa. Wanasayansi wanasema ulimwengu ulianzishwa na mlipuko wa ‘Big Bang’, uliotokea takribani miaka bilioni 14 iliyopita, kutoka katika kitu kidogo zaidi kuliko ncha ya sindano, lakini hawatuambii nini kilisababisha mlipuko huo utokee au hicho kitu kidogo kuliko ncha ya sindano kilitoka au kilikuwa wapi.

Wanaendelea kusema kuwa baada ya ‘Big Bang’ kutakuwepo na ‘Big Crunch’, ambapo ulimwengu utarudia hali yake ya awali ya udogo kuliko ncha ya sindano, na kila kitu kinachoonekana leo ulimwenguni hakitaonekana tena.

Hapo sasa ndipo utata unapokuja. Mlipuko wa ‘Big Bang’ ulipotokea ulimwengu ulilipuka na kusambaa pande zote nne za ulimwengu kwa mwendokasi wa zaidi ya kilometa milioni 2 kwa saa, mpaka hivi leo unavyoonekana na bado unaendelea kusambaa. Kutokana na dhana ya ‘Big Crunch’, wanasayansi wanaamini ulimwengu utapanuka ila baadaye utapungua mwendo na utarudi mwanzo kabisa mahali ulipolipukia.

Lakini mwaka 1995 wanasayansi hao hao waligundua kitu. Ulimwengu – badala ya kupungua mwendo wa kupanuka kama wanasayansi walivyokuwa wakitabiri – sasa unaongeza mwendo, tena kwa mwendokasi ambao haujawahi kutokea.

Hiki ni nini kinachosababisha ulimwengu uongeze mwendokasi kiasi hicho badala ya kuupunguza? Hicho ni nini ambacho ulimwengu unapanukia? Wanasayansi hawana jibu. Wanasingizia kitu kinaitwa ‘dark matter’, maada ambayo haijawahi kuonekana, kwamba ndicho kinachosababisha ulimwengu uongeze mwendokasi kwa kiwango hicho ambacho hakijawahi kutokea; na hicho ambacho ulimwengu unapanukia wanahisi ulimwengu wetu unapanukia katika ulimwengu mwingine, kwa mujibu wa dhana nyingine kabisa iitwayo ‘multiverse’ au ‘meta-universe’.

Kuna kitu kinaitwa ‘Higgs boson’ – chembe ndogo inayosemekana kuhusika na uzito (‘mass’) wa chembe ndogo 16 zilizomo ndani ya atomu, kasoro chembe ya mwanga, iliyopotea mara tu baada ya mlipuko wa ulimwengu wa ‘Big Bang’ miaka bilioni 13.7 iliyopita katika kipindi kilichoitwa ‘epoch’ – ambayo ilianza kutafutwa katika maabara za CERN, Uswisi, toka mwaka 1964, maabara ambazo kazi yake kubwa ni kutengeneza mazingira ya mwanzo kabisa ya mlipuko wa ‘Big Bang’, kusudi wanasayansi waone kama wanaweza kubahatisha kuiona na kuidhibiti hiyo bosoni.

Bosoni itakapopatikana wanasayansi watajua siri ya ‘dark matter’, watajua jinsi ulimwengu unavyofanya kazi na jinsi ulivyoumbwa na jibu la kitendawili cha ‘Standard Model’ litapatikana.

Hiyo ni kazi ngumu. Ndiyo maana ‘Higgs boson’ mwaka 1993 iliitwa ‘The God Particle’. Yaani, wanasayansi wanahisi kuna muujiza wa Kimungu na huenda wasiipate kabisa hiyo bosoni. Wanasema waliipata mwaka 2013. Lakini hiyo waliyoipata bado ina utata.

Kutokana na kushindwa huko kwa sayansi na historia, kutokana na kushindwa kwa sayansi kutengeneza binadamu au mnyama, kutokana na miujiza iliyorekodiwa katika vitabu vitakatifu; naamini, Mungu yupo.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Wanasayansi wana uwezo wa kupeleleza hadi kipindi cha karne ya kwanza ambapo Yesu aliishi, alikufa, alifufuka na alipaa kwenda mbinguni, na wana uwezo wa kujua mambo mengi kwa hakika yaliyofanyika katika kipindi hicho na hata katika kipindi cha kabla ya hapo.

Kuna miujiza ambayo Yesu aliifanya ambayo haiko ndani ya Biblia. Kwa mfano, Biblia inasema Yesu alizaliwa ndani ya zizi la ng’ombe wakati sayansi inasema alizaliwa nje ya zizi la ng’ombe; na muujiza wa kwanza kuufanya ambao hauko ndani ya Biblia ni kutembea mara tu baada ya kuzaliwa, na watu na ndege wa angani kuganda kabla ya kuzaliwa Masihi na kabla ya wakunga kufika kumsaidia Maria Magdalena kujifungua.

Akiwa na umri wa miaka sita, sayansi inasema, Yesu alikuwa akicheza na mtoto mwenzake juu ya paa la nyumba ya jirani na mara Yesu akamsukuma mwenzake kutoka juu hadi chini na mwenzake huyo akafariki papo hapo. Watu walipomsonga sana Yesu kwa kumtuhumu kuwa yeye ndiye aliyesababisha kifo cha mwenzake, na kwamba wangemfungulia mashtaka, Yesu alikataa katakata kuhusika na kifo hicho.

Lakini walipozidi kumsonga, aliusogelea mwili wa rafiki yake kisha akamwita na kumwambia asimame. Yule mtoto alisimama! Huo ukawa muujiza mkubwa wa kwanza wa Yesu Kristo, kufufua mtu nje ya maandiko matakatifu.

Kuna mifano mingi inayodhihirisha uwepo wa Mungu ambayo wanasayansi hawawezi hata kuipatia majibu. Tukio la Yoshua kusimamisha jua limewashangaza wanasayansi hadi nyakati za leo. Mwanzoni mwa miaka ya 70 wanasayansi walijaribu kurudisha muda nyuma kwa kompyuta kuona kama kweli wangekuta takribani siku moja imepotea kama ilivyorekodiwa katika Biblia.

Cha kushangaza, cha kushangaza mno, walikuta saa 23 na dakika 20 zimepotea katika mazingira ambayo hawakuweza na hawataweza kuyaelewa. Walipochunguza vizuri walikuta ni kipindi cha miaka ya 1500 KK (Jumanne tarehe 22 Julai) ambacho ndicho tukio la Yoshua la kusimamisha jua na kusogeza mwezi nyuma digrii 10, ambazo ni sawa na mzunguko wa dakika 40, lilipotokea.

Kwa kutumia elimu ya wendo, elimu ya kupanga miaka na matukio ya Kibiblia, dunia iliumbwa Jumapili tarehe 22 Septemba mwaka 4000 KK. Hata hivyo, mahesabu ya kalenda yanaonyesha kuwa Septemba 22 ilikuwa Jumatatu (si Jumapili) na kwamba kosa hilo labda lilisababishwa na siku ya Yoshua iliyopotea.

Hayo yote ni kwa mujibu wa Profesa C. A. Totten, wa Chuo Kikuu cha Yale, katika kitabu chake cha ‘Joshua’s Long Day and the Dial of Ahaz: A Scientific Vindication and a Midnight Cry’ kilichochapishwa mwaka 1890.

Kama hakuna Mungu iliwezekanaje Yoshua aombe jua lisimame na jua likasimama kweli? Iliwezekanaje Yesu aseme atakufa, atafufuka na atapaa kwenda mbinguni na kweli ikatokea kama alivyosema? Ndani ya Biblia kuna tabiri 333 zilizotabiri maisha yote ya Yesu Kristo hapa duniani na zote zilitimia – bila kupungua hata moja. Utasemaje hapo hakuna Mungu? Mungu yupo, naamini, sijui.

Tukio la Yesu kufa, kufufuka na kupaa kwenda mbinguni si la vitabu vitakatifu pekee, hata sayansi inakubaliana na hilo.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Damu ya Yesu Kristo ina nguvu katika ulimwengu wowote ule uliowahi kuumbwa na Mwenyezi Mungu. Itumie!”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ukiwaza kitu kwa dakika moja na sekunde nane – huu ni utafiti wangu tu – hicho kitu kitaanza kujiumba kwa ajili yako sehemu fulani ulimwenguni. Ukiamini kwa kiasi cha kutosha kwamba umekipata, utakipata. Haijalishi kama una elimu au huna. Hiyo ndiyo siri kubwa zaidi ya utajiri kuliko zote duniani – MAWAZO YAKO.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ukifuata kanuni ya nguvu ya uvutano uhitaji kujua jinsi utakavyofanikiwa. Kazi yako ni kuwaza tu kwa namna inavyotakiwa. Waza na amini kwa asilimia mia moja. Mengine yote mwachie Mungu au ulimwengu. Mungu pekee ndiye anayekupa njia na bahati, ili wewe ufanikiwe. Atakupa nguvu ya kufanya kazi na ujanja wowote utakaohitajika, katika harakati hizo za mafanikio yako.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Tuko peke yetu ulimwengu mzima halafu bado tunagombana na kudharauliana!”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Lazima kuna mtu, si kitu, mwenye akili ya kupindukia, aliyeanzisha kila kitu kinachoonekana ulimwenguni. Mwaka 1995 wanasayansi waligundua kitu kilichowashtua kuliko kitu kingine chochote kile katika historia ya uwepo wao. Waligundua kuwa ulimwengu unaongeza mwendo wa kupanuka katika pande zote nne za ulimwengu – kwa mwendokasi wa maili milioni mbili kwa saa! Nini kinasababisha ulimwengu uongeze mwendo kiasi hicho badala ya kuupunguza? Ni nini hicho ambacho ulimwengu unapanukia? Mpaka sayansi ijibu maswali hayo na mengineyo mengi, kama vile kitendawili cha ‘standard model’ na chembe ya ‘boson’ inayofanya kila kitu ulimwenguni kuwa na uzito, nitaendelea kuamini kuna Mtu anayesababisha yote hayo kutokea.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Hata hivyo, toka mwaka 1995 watu wengi walianza kuamka kiroho dunia nzima; na mwaka 2012 waliamka zaidi, pale ulimwengu ulipoanza kuhama kutoka kwenye masafa ya ngazi ya nne ya ufahamu wa binadamu (‘4th dimension’) kwenda kwenye masafa ya ngazi ya tano ya ufahamu wa binadamu (‘5th dimension’) inayohusika zaidi na ulimwengu wa roho na ambayo bado inaendelea kuhama mpaka dakika hii. Ndiyo maana watu wengi zaidi wanamjua Mungu kipindi hiki kuliko kipindi kingine chochote kile katika historia ya dunia yetu. Kwa sababu hiyo, Shetani hatashinda.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Umeufanyia nini ulimwengu?”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kwa sababu ya kutofautiana kati ya Mungu na ulimwengu huu, dunia hii haiwezi kuwa dunia ambayo Mungu alijitolea Mwanawe wa pekee.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Maisha ni kitu cha ajabu kuliko vyote ulimwenguni kilichowashangaza hata wanasayansi wa dunia hii. Amka na uujue ukweli.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Unapoupinga utafiti wa mtu upinge kwa utafiti mwingine! Bila hivyo unashindana na ulimwengu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ukiropoka unashindana na ulimwengu! Kiri, ikiwa umekosa, na tubu.”
Enock Maregesi