Fonimu
Mandhari
Fonimu ni jina linalotumiwa katika elimu ya fonolojia kwa kutaja sauti bainifu za lugha fulani zilizo sehemu ndogo kabisa za maneno na kuunda tofauti za maana kati ya neno moja na jingine.[1]
Katika Kiswahili
[hariri | hariri chanzo]Katika lugha ya Kiswahili tunaweza kutofautisha fonimu za aina tatu:
- Fonimu za irabu ambazo ni a - e - i - o - u
- Fonimu za nusuirabu ambazo ni w - y
- Fonimu za konsonanti ambazo zinaonyeshwa kwa herufi za b - ch - d - dh - f - g - gh - h - j- k - kh - l - m - n - ny - ng' - p - r - s - sh - t - th - v - z; baadhi zinaonyeshwa kwa kuunganisha herufi mbili kama vile dh - kh - ng - ng`- th.
Wataalamu wanatofautiana juu ya idadi ya fonimu za Kiswahili kama ni kwa jumla 33 au 37. [2].
Fonimu huweza kubadili maana ya neno katika lugha husika.
- mf.-[punga], hapa fonimu [p] ikibadilishwa na kuwekwa fonimu nyingine maana ya neno la awali hubadilika.
- mf.-[tunga] fonimu [t] imebadili maana ya neno la awali punga
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Concise Oxford English dictionary
- ↑ Susan Choge, Understanding Kiswahili Vowels, in The Journal of Pan African Studies, vol.2, no.8, Machi 2009, pp 62-77
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Fonimu kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |