Nenda kwa yaliyomo

Maria kutolewa hekaluni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 12:50, 28 Oktoba 2024 na Riccardo Riccioni (majadiliano | michango)
(tofauti) ← Pitio lililotangulia | Toleo la sasa (tofauti) | Pitio linalofuata → (tofauti)
Mchoro wa ukutani huko Skopje, Macedonia.
Mchoro wa Titian (1534-1538, Gallerie dell'Accademia, Venice).

Bikira Maria Kutolewa Hekaluni ni kumbukumbu ya liturujia inayoadhimishwa na Wakatoliki na Waorthodoksi tarehe 21 Novemba[1][2].

Adhimisho linatokana na habari ambayo haipatikani katika Agano Jipya, ila katika Injili ya Yakobo. Humo inasimuliwa kwamba wazazi wa Bikira Maria, Yohakimu na Ana, ambao hawakuwa na watoto, walipata ujumbe kutoka mbinguni kwamba watapata mtoto.

Kama shukrani ya kupata mtoto wa kike, akiwa bado mdogo walimleta katika Hekalu la Yerusalemu ili kumweka wakfu kwa Mungu[3].

Huko alibaki hadi alipotolewa kwa Yosefu.[3][4]

Kwa namna nyingine, inaaminika kwamba mwenyewe alijitoa mapema kwa Mwenyezi Mungu, yeye aliyejaa neema tangu kutungwa mimba kwa kukingiwa dhambi ya asili na atakayejaliwa kuwa Mama wa Mungu kwa uwezo wa Roho Mtakatifu [5].

Sikukuu ilianzishwa kuhusiana na kutabaruku Basilika jipya la Mtakatifu Maria, lililojengwa mwaka 543 na kaisari Justinian I karibu na mabaki ya Hekalu la Yerusalemu.[4]

Kutoka Ukristo wa mashariki sikukuu ilienea katika monasteri za Italia Kusini katika karne ya 9, ikaingia katika liturujia ya Papa wa Avignon mwaka 1372 kwa agizo la Papa Gregori XI.[6][7]

  1. Martyrologium Romanum
  2. Some but not all Eastern Rite churches reckon by the Julian calendar, in which this date falls 13 days later on December 4 of the Gregorian calendar.
  3. 3.0 3.1 "Peters, Sr. Danielle. "The Holy Land: In the Footsteps of Mary of Nazareth", Marian Library, University of Dayton". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-06-12. Iliwekwa mnamo 2016-10-14.
  4. 4.0 4.1 "Mauriello, Matthew R., "November 21: Presentation of Mary", Fairfield County Catholic, 1996". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-10-03. Iliwekwa mnamo 2016-10-14.
  5. https://www.santiebeati.it/dettaglio/25200
  6. "The Saint Andrew Missal, with Sundays and Feasts," by Dom Gaspar LeFebvre, O.S.B., Saint Paul, MN: The E. M. Lohmann Co., 1952, p. 1684
  7. William E. Coleman, Ed. "Philippe de Mezieres' Campaign for the Feast of Mary's Presentation," Toronto: Pontifical Institute of Mediaeval Studies, 1981, pp. 3-4.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Maria kutolewa hekaluni kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.