Wavidunda
Wavidunda ni kabila la watu wa Wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro katika Mashariki-kati ya nchi ya Tanzania.
Jina linamaanisha kuwa wanaishi milimani. Mwaka 1987 idadi ya Wavidunda ilikadiriwa kuwa 32,000 Jamii katika Kabila la Wavidunda linaamini katika imani ya Dini ya Kikrsito pamoja na dini ya Kiislamu .[1]
Wavidunda wanazo ngoma za asili ambazo ni mng'wedu na siranga.
Upande wa mavazi ni nguo aina ya kaniki.
Hupendelea kuwinda kwa kufukuza wanyama kwa mbwa na mikuki.
Kabila la Wavidunda pia wanapenda sana kilimo: mazao ambayo hulimwa kwa wingi ni mahindi, maharage, mihogo, ndizi, mananasi na mengine mengi.
Chifu wa kabila hili ni chifu Ngwila, matambiko yao huongozwa na mtu mmoja katika familia hiyo ambaye hakutahiriwa. Mahali pa tambiko hilo kuu ni katika milima ya Iyunji.
Tanbihi
- ↑ Weekes, Richard V. (1984-12-21). Muslim Peoples [2 Volumes]: A World Ethnographic Survey (kwa Kiingereza). Bloomsbury Academic. uk. 104. ISBN 978-0-313-23392-0.
Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Wavidunda kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |