Waluo
Waluo (pia Wajaluo) ni kabila kutoka Sudan Kusini. Wako hasa magharibi mwa Kenya, kaskazini mwa Uganda na mashariki mwa Tanzania katika Mikoa ya Mara na Mwanza. Nchini Kenya ni kabila la nne kwa wingi wa watu (11% za wakazi wote wa nchi). Inawezekana katika nchi hizo kwa jumla wamezidi milioni 7, mbali na makabila ya jamii hiyohiyo.
Lugha yao ni Kiluo. Wenyewe hujiita Jaluo na lugha yao Dhulou.
Waluo ni mkusanyiko wa kabila la Waniloti ambalo lilisafiri kutoka Afrika ya Kaskazini kufuata mto Nile kwenda Kusini. Waluo wengi wameenea kandokando ya Ziwa Viktoria kutokana na utamaduni wao wa uvuvi.[1]. It is estimated that Dholuo has 90% lexical similarity with Lep Alur (Alur language); 83% with Lep Achol (Acholi language); 93% with Dhopadhola (Padhola language), 74% with Anuak, and 69% with Jurchol (Luwo) and Dhi-Pari (Pari).
Wajaluo mashuhuri
- Philemon Sarungi - Mtaalamu wa udaktari na kiongozi nchini Tanzania
- Gidi Gidi Maji Maji - Wasanii wa muziki aina ya hip hop
- Tom Mboya - mwanasiasa aliyeuawa mwaka 1969
- Barack Obama - mwanasiasa na Rais wa Marekani ni mwana wa baba Mjaluo
- Jaramogi Oginga Odinga - mwongozi wa Wajaluo kutoka wakati wa kupigania uhuru, mwanzilishi wa vyama vya KANU, KPU, FORD-Kenya na makamu wa rais wa kwanza
- Raila Amolo Odinga - mwana wa Jaramogi na mwanasiasa muhimu wa kitaifa
- Robert Ouko - waziri wa mambo ya nje aliyeuawa 1990.
- Daniel Owino Missiani - mwanamuziki Mtanzania aliyewahi kuwania tuzo la muziki aina ya rhumba nchini Kenya alifariki mwaka 2006 na kuzikwa Shirati Rorya
- Riaga Ogalo - mwenyekiti wa Wajaluo Afrika Mashariki
- Odemba Kagose - mtemi wa Buturi
- Ochuodho Awino - mtemi wa Kamageta
- Mirimbo Oreck Ragare - mzee wa kwanza Kamageta kununua baiskeli, alikufa mwaka 1999 katika kijiji cha Osiri.
- Daniel Opanga Oole wa Kamageta (baba wa balozi Joshua Watson Opanga) - mwanzilishi wa kanisa la Wamenonite huko Kamageta, kata ya Roche, Rorya, alifariki mwaka 1992
- Timothy Apiyo - waziri mkuu mstaafu wa Tanzania
Marejeo
- ↑ Cooper, Julien (2017). "Toponymic Strata in Ancient Nubia until the Common Era". Dotawo: A Journal of Nubian Studies. 4. doi:10.5070/d64110028.
Makala hii kuhusu utamaduni wa Kenya bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Waluo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Waluo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |