Emmett Till
Emmett Till | |
---|---|
Amezaliwa | Emmett Louis Till Julai 25, 1941 |
Amekufa | 28 Agosti 1955 (umri 14) Money, Mississippi U.S. |
Asili yake | African-American |
Elimu | James McCosh Elementary School |
Wazazi | Mamie Carthan Till-Mobley Louis Till |
Emmett Louis "Bobo" Till (25 Julai 1941 – 28 Agosti 1955) alikuwa mvulana Mmarekeni Mweusi ambaye aliuawa mjini Money,Mississippi baada ya kuonesha hali ya kimapenzi kwa mwanamke Mzungu.
Tukio la kifo
[hariri | hariri chanzo]Till alikuwa anatokea mjini Chicago, Illinois. Alienda kuwaona ndugu zake katika eneo la Mississippi Delta ambapo akiwa huko alizungumza na Carolyn Bryant mwenye umri wa miaka 21. Alikuwa muolewa wa mmiliki wa grosari ndogo mjini humo. Usiku kadhaa baadaye, mume wa Bryant, Roy na kaka yake wa kufikia aliyeitwa J. W. Milam, walienda katika nyumba ya baba yake mkubwa Till. Wakamchukua Till hadi bandani.
Inaaminika huko walimpiga na kulitoa jicho lake moja. Kisha wakampiga risasi ya kichwa na kuutupa mwili wake katika Mto Tallahatchie. Mwili wkae uliokotwa katika mto baada ya siku tatu mbele.
Mazishi
[hariri | hariri chanzo]Mwili wa Till ulirudishwa Chicago. Mama yake alitaka mazishi ya umma huku jeneza likiwa wazi. Alitaka kuuonesha ulimwengu jinsi mtoto wake alivyouawa. Maelfu ya watu walienda mazikoni hapo na kuona jeneza lake. Taswira ya mwili wake zilichapishwa katika majarida kibao ya Wamarekani Weusi na magazetini vilevile. Hili liliungwa mkono na watu weusi na weupe vilevile nchini Marekani. Hapo mwanzo, magazeti na maafsia usalama walikuwa kinyume na tukio hilo, yaani, waliona kama watendaji wameonewa wamepewe haki yao. Muda mfupi wakaanza kupata misukuosuko walipondwa na nchi nzima hasa kwa kuwatetea watu wa Mississippi kwa vitendo vyao. Hili lilipelekea watu kuanza kubwatuka na kuwaita wale wakosaji ni wauaji na si vingine.
Kesi
[hariri | hariri chanzo]Kesi ya hao walioshtakiwa kwa kosa la kumuua Till ilivuta hisia ya watu wengi mno katika jamii. Bryant and Milam waliachiwa huru, yaani, hawakukutwa na hatia yoyote ya kumuua Till. Hakuwashtakiwa kwa kumtekenyara. Miezi kadhaa baadaye, kwa vile hawawezi kushtakiwa tena hasa kwa kufuatia muundo wa kesi kwa kipindi hicho ya kwamba, kwa makusudi wakati wa mahojiano ma jarida moja wakasema walimuu Till. Mauaji ya Till huhesabiwa kama tukio muhimu lililopelekea kuanzishwa kwa Harakati za Kutetea Haki za Mtu Mweusi nchini Marekani.
Matatizo ya kuthibitisha kama kweli ule ulikuwa mwili wa Till uliathiri kesi. Hili ndilo hasa lilopelekea kufutiwa kesi kwa Bryant na Milam. Kesi ilifunguliwa upya na Kitengo cha Sheria cha Marekani mnamo 2004. Uchunguzi wa maiti ulifanyika. Ulithibitishwa kuwa ni ulikuwa mwili wa Till. Alizikwa katika jeneza jipya. Jeneza lake la zamani lilipewa kwa Taasisi ya Smithsonia.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Huie, William Bradford (January 1956). The Shocking Story of Approved Killing in Mississippi, Look Magazine. Retrieved February 2012.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Emmett Till kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |