Nenda kwa yaliyomo

Epafra

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sanamu ya Mt. Epafra.

Epafra (kwa Kigiriki Ἐπαφράς, Epafras; alifariki Kolosai, 80) alikuwa mwanafunzi na msaidizi wa Mtume Paulo katika uinjilishaji wa mji wa Efeso na mkoa wa Asia.

Inaonekana alikuwa mwenyeji wa Kolosai na alitumwa kueneza Ukristo huko (Kol 1:7; 4;12-13) pamoja na Laodikea na Yerapoli.

Baada ya muda, yalijitokeza huko matatizo ya kiimani yaliyomfanya Paulo aandike barua maarufu kama Waraka kwa Wakolosai.

Paulo anamtaja pia kama mfungwa mwenzake (Waraka kwa Filemoni 1:23).

Kwa jinsi alivyomsifu, kama mshiriki mpenzi wa kazi yake na mtumishi mwaminifu wa Kristo, tangu kale anaheshimiwa na madhehebu mengi kama mtakatifu[1].

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 19 Julai[2].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Epafra kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.