Nenda kwa yaliyomo

Imani sahihi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kanuni ya Imani ya Nisea ni kigezo kimojawapo cha kupimia usahihi wa imani katika Ukristo.

Imani sahihi (kwa Kiingereza Orthodoxy, kutoka maneno ya Kigiriki orthos + doxa,[1]) ni msimamo unaokubali mafundisho sanifu ya dini fulani, tofauti na yale ya wachache.[2]

Umuhimu wa jambo hilo unasisitizwa hasa katika dini inayokiri umoja wa Mungu, lakini si katika dini nyingine kama zile za jadi au za miungu mingi.

Katika Ukristo, inamaanisha kwa kawaida kukubali imani kama ilivyofundishwa na mitaguso ya kiekumene katika karne za kwanza za dini hiyo dhidi ya uzushi wa aina mbalimbali.[1]

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Matumizi ya neno hilo yanashuhudiwa kwanza na Codex Iustinianus (Mkusanyo wa Justiniani I) ya miaka 529-534, inayodai majimbo yote duniani yawekwe chini ya maaskofu waliokubali kanuni ya imani ya mtaguso mkuu wa Nisea[3][4]

Baada ya farakano la mwaka 1054 kati ya Kanisa la Kilatini na Makanisa ya Mashariki ambayo yalikuwa bado na ushirika na Papa wa Roma, ingawa pande zote mbili ziliendelea kujiona ya Kiorthodoksi na ya Kikatoliki, polepole neno la kwanza limekuwa likitumiwa zaidi na Ukristo wa Mashariki na lile la pili na Ukristo wa Magharibi.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. 1.0 1.1 orthodox. Dictionary.com. Online Etymology Dictionary. Douglas Harper, Historian. Dictionary Definition (accessed: March 03, 2008).
  2. orthodox. Dictionary.com. The American Heritage Dictionary of the English Language, Fourth Edition. Houghton Mifflin Company, 2004. Dictionary definition (accessed: March 03, 2008).
  3. Liddell & Scott; Code of Justinian: "We direct that all Catholic churches, throughout the entire world, shall be placed under the control of the orthodox bishops who have embraced the Nicene Creed."
  4. Jostein Ådna (editor), The Formation of the Early Church (Mohr Siebeck 2005 ISBN 978-316148561-9), p. 342
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Imani sahihi kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.