Nenda kwa yaliyomo

Juma Kaseja

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Juma Kaseja
Maelezo binafsi
Jina kamiliJuma Kaseja Juma
tarehe ya kuzaliwa20 Aprili 1985 (1985-04-20) (umri 39)
mahali pa kuzaliwaTanzania
Maelezo ya klabu
Klabu ya sasaKMC
Youth career
2008–2010Makongo Dar es Salaam
Serengeti Boys
Senior career*
MiakaTimuApps(Gls)
2000–2003Moro United
2003–2014Simba
2014–2015Young Africans
Mbeya City
Kagera Sugar
KMC F.C.
Timu ya Taifa ya Kandanda
2001–2007Tanzania{{{nationalcaps(goals)1}}}
2009–presentTanzania (recalled){{{nationalcaps(goals)2}}}
* Senior club appearances and goals counted for the domestic league only and correct as of 3 July 2014.

† Appearances (Goals).

‡ National team caps and goals correct as of 3 July 2014

Juma Kaseja, (alizaliwa 20 Aprili 1985) ni mwanasoka Mtanzania ,anayecheza nafasi ya golikipa wa klabu ya KMC FC. Pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars).

Mwanzoni Kaseja, alitumikia klabu ya Simba S.C., na aliondoka muda mfupi tu baada ya msimu kumalizika. Katika umri wake mdogo alichezea timu ya Makongo Dar es Salaam na Serengeti Boys Timu ya vijana ya Tanzania. Mnamo mwaka 2000 .Kaseja alijiunga na klabu ya Moro United F.C.

Kazi katika ngazi ya Klabu

[hariri | hariri chanzo]

Katika kukua kwake, Kaseja alisoma shule ya sekondari Makongo. Alifanikiwa kucheza katika chama cha mpira wa miguu cha Makongo Dar es Salaam. Uwezo aliouonesha katika uchezaji wake ulifuatiwa na kuteuliwa kuichezea timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17.[1]

Kabla ya msimu wa 2000-2001, Kaseja alijiunga na Moro United F.C. iliyokua ikicheza ligi ya taifa ya ATnzaania (Tanzanian football). Alicheza kwa misimu miwili kabla ya kupigwa marufuku kucheza na shirikisho la soka Tanzania TFF (Tanzania Football Federation), marufuku hyo ilitokana na kitendo cha Kaseja kwenda kushiriki Gothia Cup, mashindano ya timu za vijana huko nchini Sweden. Badda ya tukio hilo, Juma Kaseja alijiunga na klabu ya Simba S.C. iliyokua ikishiriki ligi kuu ya Tanzania bara Tanzanian Premier League. Alitumikia klabu ya simba kuanzia mwaka 2009, Novemba 11, 2013, Kaseja alisajiliwa na klabu ya Yanga (Young Africans S.C.), miongoni mwa klabu zinazofanya vizuri katiak ligi ya Tanzania bara. Uhamisho huo ulionekana kama changamoto na wengi mkutokana na ushindani na utani baina ya klabu hzo mbili.[2][3]

Kazi kimataifa

[hariri | hariri chanzo]

Kaseja anaitumikia timu ya taifa ya Tanzania(Tanzania) katika michezo ya kimataifa. Alijiunga na timu ya taifa mwaka 2001 na alikua mlinda lango namba mbili wa timu. Kaseja alifanikiwa kuwa kipa namba moja baada ya mi9simu michache tu lakini aliachwa kwenye kikosi cha timu ya taifa kwa kipindi ya takribani mi9aka mitatu. Kwa kiwango alichokua nacho alifanikiwa kumshawishi kocha kutokea Denmark, Jan B. Poulsen kumrudisha katika kikosi chake, kocha huyo aliwahi kuzifundisha timu za mataifa tofauti zikiwemo timu taifa ya Armenia na ile ya Singapore , baada ya kurudishwa katika timu ya taifa, uwezo wake ulitia wengi shaka baada ya kupata matokeo mabaya inayokumbukwa zaidi ni dhidi ya timu ya Moroko , katika michezo mitatu ambayo yote Tanzania ilipoteza, alifungwa jumla ya magoli saba.[4] Katika mashindano ya CECAFA, ya mwaka 2010 (2010 CECAFA Cup) ambayo Tanzania walikua wenyeji, Kaseja aliisaidai Tanzania kushinda taji la mshindi wa tatu. Baada ya kuifunga timu ya taifa ya Ivory Coast. Uwezo wa Kaseja ulifadhaisha wengi katika michuano ya CECAFA ya mwaka 2012 (2012 CECAFA Cup), katika mchezo wa nusu fainali dhidi ya timu ya taifa ya Uganda , Kaseja alifanya kosa lililogharimu timu baada ya kushindwa kuokoa mpira uliochezwa na Robert Ssentongo.[5]

  1. Okinyo, Collins. "Up close with Simba keeper Juma Kaseja". SuperSport.com. Iliwekwa mnamo 4 Julai 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Ayo, Millard. "Unataka kuona picha za Juma Kaseja akisaini kujiunga Yanga na kiwango cha pesa kilichotolewa kumchukua?". MillardAyo.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 14 Julai 2014. Iliwekwa mnamo 2 Julai 2014. {{cite web}}: Unknown parameter |deadurl= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Football: Juma Kaseja". FootballDatabase.eu. Iliwekwa mnamo 2 Julai 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "Football - national team: Maroc". FootballDatabase.eu. Iliwekwa mnamo 3 Julai 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. Moseti, Brian. "It's Uganda and Kenya in CECAFA finals". Futaa.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-12-09. Iliwekwa mnamo 7 Juni 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Juma Kaseja kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.