Nenda kwa yaliyomo

Kampuni ya Magazeti ya Community

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kampuni ya Magazeti ya Community
Jina la kampuni Kampuni ya Magazeti ya Community
Ilianzishwa Januari 1991
Huduma zinazowasilishwa Uchapishaji
Mmiliki GateHouse Media
Aina ya kampuni Kampuni inayomilikiwa na Umma
Makao Makuu ya kampuni 254 Second Avenue
Needham
Massachusetts 02494
Bidhaa zinazosambazwa na kampuni hii *.Magazeti ya kila siku
*.Magazeti ya kila wiki
Nchi Marekani Marekani
Tovuti http://wickedlocal.com

Kampuni ya Magazeti ya Community(Community Newspaper Company - CNC), ni kampuni ndogo shirika ya GateHouse Media ambayo huchapisha magazeti katika eneo la mashariki ya Massachusetts. Ilianzishwa katika mwaka wa 1991 kama kampuni ya kuendesha kampuni kadhaa za uchapishaji na ikanunuliwa na Fidelity Investments katika mwaka wa 2001. Fidelity iliiuza kampuni hii kwa Boston Herald katika mwaka wa 2006.Kampuni hii ambayo ni mnyororo mkubwa wa kampuni kadhaa na inajulikana kama Wachapishaji Wakubwa kabisa wa magazeti ya kila wiki katika eneo la New England ilinunuliwa na GateHouse Media na ikawa sehemu kubwa kabisa ya GateHouse Media.

Jarida maarufu kabisa la CNC ni The MetroWest Daily News ambalo lina makao yake Framingham, Massachusetts. Magazeti matatu mengine ya Daiily News katika maeneo ya Boston ,pia, yanamilikiwa na CNC.

Tangu katikati mwa mwaka wa 2006, CNC na kampuni mbili shindani zilinunuliwa na GateHouse Media. Magazeti ya kila siku ya CNC na ya kila wiki yamekuwa yakifanya kazi pamoja na gazeti la The Enterprise katika Brockton na The Patriot Ledger katika Quincy. Hivi majuzi, gazeti liliunda uhusiano mwema na gazeti la The Herald News ya Fall River na Taunton Daily Gazette ambayo ni majarida yaliyonunuliwa na kampuni ya GateHouse. Magazeti haya manne yaliendelea kufanya kazi katika usimamizi wao wa wa zamani lakini hawahesabiwi kama sehemu ya Kampuni ya Magazeti ya Community(CNC).

Magazeti

[hariri | hariri chanzo]

CNC inachapisha zaidi ya magazeti 100: ya kila wiki, ya kila nusu wiki na ya kila mwezi. Kila chapisho linaorodheshwa katika moja ya vitengo vitano, ambavyo kila kimoja kina Mhariri wake Mkuu. Vitengo vinahusisha maeneo ya kijiografia mashariki mwa Massachusetts na vina majina yao kulingana na eneo lao katika Boston.

Kitengo cha Magharibi kinaendesha magazeti yote manne ya kila siku, yakiongezwa kwa magazeti ya kila wiki yanayochapishwa na CNC; kitengo cha Kusini kinahusisha magazeti kadhaa ya kila wiki yanayoshindana na magazeti mengine manne ya kila siku ya GateHouse Massaachusetts.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]