Kishawishi
Kishawishi ni tendo la kumvuta binadamu kutenda jambo. Mara nyingi maana yake ni mbaya, yaani ni kumvuta atende dhambi.
Kishawishi kinaweza kujianzia au kutokana na watu wengine, lakini dini, kama vile Ukristo, zinaweza kuona nyuma yake hasa uwepo wa nguvu za giza, hususan shetani au ibilisi.
Kishawishi chenyewe si dhambi, ila kama mtu akikikubali na kukifuata kwa hiari.
Katika Biblia
[hariri | hariri chanzo]Biblia inasema sana kuhusu kishawishi na namna ya kukishinda. Vielelezo viwili, hasi na chanya, ni vile vya Adamu na Eva upande mmoja na Yesu Kristo upande mwingine.
Adamu na Eva
[hariri | hariri chanzo]Katika Biblia kishawishi cha kwanza kiliwapata na kuwashinda Adamu na mke wake Eva. Tukio hilo maarufu kwa jina la dhambi ya asili limeathiri binadamu wote.
Yesu
[hariri | hariri chanzo]Injili zinasimulia pia vishawishi vilivyompata Yesu, hasa vitatu vilivyosababishwa na shetani jangwani, ambavyo Yesu alivishinda moja kwa moja na hivyo kutuelekeza namna ya kuvishinda vilevile.
Yesu alishawishiwa na Shetani kwa kuwa ni mtu kweli, akamshinda kwa niaba ya watu wote, akituonyesha namna ya kumtii Mungu moja kwa moja, “hata mauti, naam, mauti ya msalaba” (Fil 2:8).
“Kwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi, kadhalika kwa kutii kwake mmoja watu wengi wameingizwa katika hali ya wenye haki” (Rom 5:19).
Baba Yetu
[hariri | hariri chanzo]Sala ya Baba Yetu ambayo Yesu aliwafundisha mitume wake inamalizika kwa kuomba ushindi dhidi ya vishavishi na ya Yule Mwovu (Math 6:13).
Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |