Lamine N'Diaye
Lamine N'Diaye (alizaliwa Thiès, Oktoba 18, 1956) ni mwanasoka kutoka nchini Senegal ambaye kwa sasa ni Kocha wa Klabu ya TP Mazembe.
Uchezaji Mpira
[hariri | hariri chanzo]N'Diaye alicheza nafasi ya kiungo. Alizitumikia timu za US Rail, SC Orange, Cannes na Mulhouse, alicheza pia timu ya taifa ya mpira wa miguu ya Senegal.[1]
Ukocha
[hariri | hariri chanzo]Mwaka 1998, N'Diaye aliifundisha klabu ya Mulhouse kwa muda mfupi.[2] Baadaye alihama na kufundisha klabu ya Coton Sport kuanzia mwaka 2003 mpaka 2006.[3] Mnamo January 2008, alikabidhiwa kikosi cha timu ya taifa ya Senegal, hii ni baada ya Henryk Kasperckzak kujiuzulu.[4] Mwaka huohuo mnamo Oktoba, alifutwa kazi ya kufundika timu ya Taifa.[5] Ilipofika Disemba 2008, N'Diaye aliteuliwa kuwa Meneja wa klabu ya nchini Moroko Maghreb Fez, na mwaka 2010 mwezi September, alipata kazi ya kufundika klabu ya TP Mazembe.[3] Mnamo Mei 2013, alibadili nafasi na kuwa mkurugenzi wa ufundi wa TP Mazembe.[6] Alipoondoka Mazembe 2014, alijiunga na AC Léopards kama Mkurugenzi wa Ufundi.[7] Ilipofika Julai 2018, akachukua nafasi ya Meneja kwenye klabu ya Al-Hilal.[8] Kazi ya kukinoa kikosi cha HoroyaAC alianza Novemba 2019.[9]
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Lamine N'Diaye at National-Football-Teams.com
- ↑ "France - Trainers of First and Second Division Clubs". RSSSF. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 31 Mei 2008. Iliwekwa mnamo 15 Oktoba 2008.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 3.0 3.1 Patrice Chitera (8 Septemba 2010). "African club champions Mazembe appoint Ndiaye as coach". BBC Sport. Iliwekwa mnamo 9 Septemba 2010.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Senegal coach Kasperczak resigns". BBC Sport. 28 Januari 2008. Iliwekwa mnamo 15 Oktoba 2008.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Piers Edwards (14 Oktoba 2008). "Senegal coach Ndiaye fired". BBC Sport. Iliwekwa mnamo 15 Oktoba 2008.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Mazembe switch Ndiaye from coach to technical director". BBC Sport. 8 Mei 2013.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "CONGO :: Lamine N'Diaye nouvel entraîneur de l'AC Léopards de Dolisie". www.camer-sport.be. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-07-19.
- ↑ "CAF - News Center - News - NewsDetails". www.cafonline.com.
- ↑ "Senegal's Lamine Ndiaye appointed new Horoya coach", BBC Sport, 12 November 2019.
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Lamine N'Diaye kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |