Nenda kwa yaliyomo

Mindanao

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha ya ramani kuonesha eneo la Mindanao
Wavuvi wa Mindanao

Mindanao ni kisiwa kikubwa cha pili katika Ufilipino ambayo ni nchi ya visiwa. Eneo la visiwa ni km² 97,530. Kuna wakazi milioni 22. Mji mkubwa ni Davao yenye wakazi milioni 1.5.

Jina hili latumiwa pia kutaja kundi la visiwa vya Ufilipino linayojumlisha kisiwa kikubwa cha Mindanao pamoja na funguvisiwa la Sulu.

Jiografia

[hariri | hariri chanzo]

Mindanao ni kisiwa ambacho kipo mashariki kabisa mwa eneo la Ufilipino na karibu zaidi na Borneo.

Asili ya kisiwa hiki kama Ufilipino wote ni ya kivolkeno; ni sehemu ya milima ya kivolkeno iliyokua kuanzia vilindi vya bahari juu ya "pete ya moto" kando ya bamba la Pasifiki.

Uso wa Mindanao ni ufuatano wa safu za milima na mabonde kati yake. Magma na majivu ya kivolkeno vilijaza mabonde kadhaa na kuwa nyanda za juu zenye sehemu za tambarare. Pwani huwa pia vipande vya tambarare vinavyokatwakatwa na milima inayoelekea hadi baharini.

Mlima mkubwa ni Apo unaofikia kimo cha mita 2,954, ni pia mlima mkubwa wa Ufilipino.

Kuna malighafi nyingi ambazo hajakutumiwa kiuchumi kutokana na ugumu wa mawasiliano na hali ya kisiasa kisiwani hasa uhaba wa usalama kutokana na uasi wa wakazi Waislamu dhidi ya serikali.

Wakazi wanatumia lugha mbalimbali. Watu wa kusini mwa kisiwa ni zaidi Waislamu walio theluthi 1 ya wakazi wa Mindanao. Sehemu kubwa zaidi ya 60% ni Wakristo, hasa Wakatoliki. Vikundi vidogo vilitunza dini na tamaduni asilia.