Monrovia
Jiji la Monrovia | |
Nchi | Liberia |
---|
Monrovia ni mji mkuu wa Liberia. Eneo uliko mji huu mwanzoni liliitwa Cape Mesurado na Wareno katika miaka ya 1560. Eneo hili lilianzwa kujenga mji mwaka 1822 na chama cha American Colonization Society ikiwa ni makazi ya watu waliokombolewa toka utumwani nchini Marekani.[1] Jina Monrovia lilitokana na jina la Rais wa Marekani James Monroe. Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2003, Mji huu una wakazi wapatao 572,000.
Uchumi wa Monrovia unategemea zaidi bandari yake na madini ya chuma. Bidhaa kama vile saruji, mafuta, matofali, vigae, samani, na kemikali zinatengenezwa Monrovia.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Wakati mabaharia Wareno walipowasilia Monrovia na kuuita mji huu "Cape Mesurado" tayari kulikuwa na wakazi wakiishi hapo. Watu wa kwanza kuhamia Monrovia toka nchini Marekani waliwasili mwaka 1822 katika Kisiwa cha Sherboro nchini Sierra Leone. Wahamiaji wengi walifariki baada ya kuwasili Monrovia.
Mkutano wa kutunga katiba ya Liberia wa American Colonization Society ulifanyikia Monrovia mwaka 1845.