Nenda kwa yaliyomo

Soyuz

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Soyuz jinsi ilivyoonekana angani.

Soyuz (kwa Kirusi Союз kwa maana ya "Umoja") ni jina la vyombo vya anga-nje vilivyobuniwa kwa ajili ya mradi wa usafiri wa anga-nje wa Umoja wa Kisovyeti.

Vilirushwa kwa kutumia roketi ya Soyuz ambayo ni chombo kilichobeba mizigo mingi angani kushinda roketi zote nyingine.[1] Soyuz zote zilirushwa kutoka kituo cha kurushia roketi cha Baikonur (leo nchini Kazakhstan).

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Soyuz ya kwanza ilirushwa angani bila rubani kama jaribio tarehe 28 Novemba 1966.

Safari ya kwanza yenye rubani iliitwa Soyuz 1 kwenye tarehe 23 Aprili 1967 lakini chombo kilianguka wakati wa kurudi kwa sababu parachuti ilikwama, na kumuua mwanaanga Vladimir Komarov. Safari ya Soyuz 3 [2] kwenye 26 Oktoba 1968 ilikuwa safari ya kwanza iliyofanikiwa. Hadi mwaka 2021 Soyuz inatazamwa kuwa chombo salama zaidi baada ya kurushwa zaidi ya mara 140[3]. Gharama zake ni nafuu zikilinganishwa na vyombo vya mataifa mengine.[4]

Vyombo vya Soyuz vilitumika kubeba wanaanga kwenda na kurudi kutoka vituo vya angani Salyut na Mir. Tangu mwisho wa mradi wa Space Shuttle ya NASA, Marekani ilitumia pia vyombo vya Soyuz kwa kupeleka wanaanga hadi Kituo cha Anga cha Kimataifa (ISS).

Angalau chombo cha Soyuz huwekwa muda wote kwenye ISS kwa matumizi wakati wa dharura.

Kila chombo cha Soyuz kina sehemu tatu ambazo zinatenganishwa wakati wa kurudi kabla ya kushuka kwenye angahewa ya Dunia. Dambra na kitengo cha huduma huanguka tu na kuungua hewani, ilhali chumba cha kurudi hupeleka wanaanga salama hadi uso wa ardhi.

  • Kitengo cha dambra chenye nafasi kwa rubani na abiria
  • Chumba kidogo cha kurudi ambamo wanaanga wanakaa wakati wa kurudi kwenye uso wa ardhi
  • Kitengo cha huduma chenye injini, fueli na paneli za sola.
Kitengo cha dambra (orbital module)

Kitengo cha dambra

[hariri | hariri chanzo]

Kitengo cha dambra (orbital module) kina nafasi ya kukaa kwa wanaanga wakati wa kuzunguka Dunia, pamoja na choo, nafasi ya mizigo na vifaa visivyohitajika wakati wa kurudi. Huwa pia na geti la kutoka wakati wa kuingia katika vituo vya angani. Hakirudi duniani.

Chumba cha kurudi

[hariri | hariri chanzo]
Chumba cha kurudi (return module)

Chumba cha kurudi (reentry module) hutumiwa wakati wa kuruka na kurudi duniani. Nusu ya uso wake imefunikwa kwa vigae vya kinga ya joto. Inarudi duniani kwa kutumia parachuti.

Moduli ya huduma

[hariri | hariri chanzo]
Kitengo cha huduma (service module)

Moduli ya huduma inabeba injini na paneli za sola. Inayo mifumo ya kudhibiti joto, ugawaji wa umeme, mawasiliano ya redio ya masafa marefu na telemetry ya redio. Hairudi duniani.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

*Roskosmos

  1. esa. "Soyuz launch vehicle: The most reliable means of space travel", European Space Agency. (en-GB) 
  2. "Soyuz-3 launch vehicle". www.russianspaceweb.com. Iliwekwa mnamo 2018-05-30.
  3. Soyuz:The Greatest Spacecraft Ever
  4. The best ride in the galaxy – coming back to Earth in a Soyuz