Spiridoni wa Tremetusia
Mandhari
Spiridoni wa Tremetusia (kwa Kigiriki: Ἅγιος Σπυρίδων; Askeia, Kupro, 270 hivi – Tremetusia 348) alikuwa askofu wa mji huo wa Kupro.
Tangu kale anaheshimiwa na Ukristo wa Mashariki na Ukristo wa Magharibi kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa mashariki tarehe 25 Desemba na magharibi tarehe 12 Desemba[1].
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Alipokuwa mchungaji alianza kujulikana kwa maisha yake ya kiroho. Alioa na kuzaa binti mmoja, Irene.
Alipofiwa mke wake, Spiridoni aliingia katika monasteri, na binti yake vilevile.
Hatimaye Spiridoni akawa askofu wa Tremetusia, katika wilaya ya Larnaca. Alishiriki mtaguso mkuu wa kwanza (Mtaguso wa kwanza wa Nisea (325), aliposaidia sana kupinga teolojia ya akina Ario.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Misemo ya Mababa wa Jangwani (Apophthegmata Patrum) – tafsiri ya W. Ngowi, O.F.M.Cap. – ed. Salvatorianum – Morogoro 2000 –ISBN 0-264-66350-0
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- St. Spyridon and other religious traditions on Corfu
- St Spyridon the Wonderworker, Bishop of Tremithus Orthodox icon and synaxarion
- Spyridon of Trimythountos
- Saint Spyridon
- The life of Saint Spyridon Archived 29 Agosti 2007 at the Wayback Machine.
- Holy Metropolis of Trimythous, Church of Cyprus
- Colonnade Statue in St Peter's Square
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |