Nenda kwa yaliyomo

Sululu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sululu
Sululu wa Ulaya
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Charadriiformes (Ndege kama vitwitwi)
Familia: Scolopacidae (Ndege walio na mnasaba na sululu)
Jenasi: Coenocorypha G.R. Gray, 1855

Gallinago Brisson, 1760
Limnodromus Wied-Neuwied, 1833
Lymnocryptes Boie, 1826
Scolopax Linnaeus, 1758

Sululu ni ndege wa jenasi mbalimbali katika familia ya Scolopacidae. Hata jenasi Numenius huitwa sululu, lakini jina membe linastahabiwa. Ndege hawa wana rangi zilizofifia na hawaonekani rahisi wotoni. Huruka tu wakati mtu anapowakaribia sana. Wana miguu mifupi na mdomo mrefu. Wapenda mahali majimaji na hula wadudu na nyungunyungu. Wakati wa majira ya kuzaa dume hufanya mkogo wa kubembeleza jike akishuka ghafla angani na kusabibisha manyoya maalum ya mkia kutoa uvumi kubwa. Hujenga tago kwa manyasi linalofichwa sana na jike huyataga mayai 3-4.

Spishi za Afrika

[hariri | hariri chanzo]

Spishi za mabara mengine

[hariri | hariri chanzo]