Kisw 7 New Format
Kisw 7 New Format
Kisw 7 New Format
MAELEKEZO
1. Mtihani huu una maswali 6 katika sehemu A, B na C.
2. Jibu maswali yote kama ulivyoelekezwa katika kila sehemu.
3. Majibu yote yaandikwe kwenye nafasi ziliachwa wazi katika karatasi hii
4. Epuka kufutafuta.
5. Simu za mkononi haziruhusiwi katika chumba cha mtihani.
3. Oanisha maneno ya kifungu A na yale ya kifungu B ili kuleta mantiki kwa kaundika herufi ya jibu
sahihi kutoka kifungu B katika mabano uliyopewa
KIFUNGU A JIBU KIFUNGU B
(i) Liamba ( ) A. Kikembe cha nyuki
(ii) Shule ( ) B. Alfajiri
(iii) Chakula ( ) C. – l -
(iv) Jana ( ) D. Tamaa mbaya
(v) Cha mtu mavi ( ) E. Kijerumani
Jina la Mtahiniwa: ___________________________________________________ Shule: _____________________
SEHEMU B (ALAMA 20)
4. Andika majibu sahihi katika sehemu wazi
(i) Changanua sentensi hii kwa usahihi, “Mvumilivu hula mbivu kutokana na uvumilivu wake”
________________________________________________________
(ii) Dora ni mjukuu wa mjukuu wangu. Kwa hiyo Dora ni nani kwangu? ____________________
(iii)Neno Shaghlabaghla lina konsonanti ngapi? ________________________________
(iv) Tegua kitendawili hiki, “Ana miguu ya msumeno” __________________________
(v) Je, kamusi ina sehemu kuu ngapi? ____________________________
5. Soma kwa makini habari ifuatayo kisha ujibu swali la (i) – (v)
Ama hakika, nimeamini maneno ya wahenga wetu yasemayo,“Asiyesikia la mkuu huona makuu”. Kwani, katika
siku za kisogoni nilishuhudia viongozi wetu mbalimbali wa chama na serikali pamoja na wataalamu wa hali ya
hewa bila kukata tama, wakionya kuhusu hatari za kuishi mabondeni, lakini bado familia yangu iliendelea
kukaidi ushauri huo pasi na hofu yoyote.
Hatimaye siku moja wingu kubwa mithili ya moshi mweusi lilitanda katika jiji letu, watu walionekana wakipita
huku na huku kwa hofu kuu. Loo! Ghafla ikashuka mvua kubwa ambayo ilinyesha kwa taribani siku tatu na nusu
mfululizo. Wakati tukila chajio mama yangu alisikika akisema , “Sikilizeni, kuna habari ya maafa huku
mabondeni” Taarifa ilisema hivi, “Watu zaidi ya korija moja wamepoteza maisha na wengine wapatao dazani
tatu wameachwa bila makazi kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika jiji letu.
Ilikuwa ni habari kubwa na ya kutisha, mali nyingi ziliharibiwa na maji. Laiti kama tungelisikiliza ushauri wa
wataalamu na viongozi wetu wa chama na serikali, tusingefikwa na maafa haya. Kweli, majuto ni mjukuu
Maswali
41. Mwandishi anasema, katika siku za kisogoni alishuhudia viongozi wake wakionya kuhusu hatari ya kuishi
mabondeni. Nini maana ya maneno, “Siku za kisogoni?’
________________________________________________________________________
42. Nini maana ya methali, “Majuto ni mjukuu” kama ilivyotumika katika habari hii?
_______________________________________________________________________
43. “Watu zaidi ya korija moja walipoteza maisha….”. Je, taarifa hii ilimaanisha nini?
__________________________________________________________________________
44. Kwa mujibu wa taarifa ya habari, mali nyingi ziliharibiwa na maji. Je, katika sentensi hii mtenda ni nini?
_________________________________________________________________________
45. Mwandishi anasema, “Laiti kama tungesikiliza ushauri wa viongozi wetu tusingefikwa na maafa haya”.
Je, hii ni aina gani ya sentensi?
________________________________________________________________________