Sera za kigeni
Sera za kigeni ya nchi (pia inaitwa sera ya mahusiano ya kimataifa, siasa ya nje; kwa Kiingereza: foreign policy) ni jumla ya matendo, matamko na mipango ya nchi vinavyolenga kuendeleza uhusiano wake na nchi nyingine, pamoja na jumuiya na mashirika vya nchi za nje kuhusu uchumi, siasa, jamii na jeshi.
Sera za kigeni zinabuniwa ili kusaidia kulinda maslahi ya taifa, usalama wa taifa, malengo ya kiitikadi, na mafanikio ya kiuchumi. Hii inaweza kufanyika kama matokeo ya ushirikiano wa amani na mataifa mengine, au kwa njia za kutisha hadi kutumia nguvu ya kijeshi.
Kwa kawaida sera ya kigeni huongozwa na waziri mkuu na waziri wa mambo ya nje. Katika baadhi ya nchi bunge pia lina jukumu kiasi la kuzisimamia.
Katika nchi mbalimbali, hasa zenye Serikali ya kiraisi, mkuu wa nchi ana jukumu kwa sera za kigeni, wakati mkuu wa serikali hasa anahusika na sera ya ndani.
Nadharia ya mahusiano ya kimataifa
[hariri | hariri chanzo]Taaluma inayoshughulika na utafiti wa mahusiano ya kigeni hujulikana kama uchambuzi wa sera za kigeni (Foreign Policy Analysis).
Angalia pia
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Makala ya Sera za Kigeni
- Muungano wa Sera za Kigeni
- Mkutano wa Masuala ya Kimataifa
- Kufundisha Sera ya Kigeni katika Enzi za Baada ya Vita Baridi Archived 5 Aprili 2010 at the Wayback Machine.
- Kamati ya Kitaifa ya Sera za Kigeni za Marekani
- Masomo ya Sera za Kigeni katika Taasisi ya Brookings
- Marejeo ya Siasa za Dunia: Nakala ya Kila Siku ya Sera za Kigeni na Usalama wa Kitaifa
Makala hii kuhusu mambo ya siasa bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |